User Rating: 2 / 5

Star ActiveStar ActiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Naibu Waziri wa TAMISEMI,Mhe. Suleiman Jaffu ametembelea banda la maonyesho ya NANE NANE katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma na kupongeza hatua za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF kupunguza umaskini nchini.

Akiwa katika banda lililoko kwenye jingo la ofisi ya Rais, Mhe. Jaffu amepata maelezo kutoka kwa baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya uzalishaji mali vilivyowezeshwa na TASAF na kujionea bidhaa zilizozalishwa na vikundi kutoka mikoa ya Manyara,Dodoma,Pwani na Singida.

 Baadhi ya bidhaa alizoonyeshwa katika banda hilo la TASAF ni pamoja na sabuni na mafuta yaliyotengenezwa kwa zao la mwani, mafuta ya alizeti ,asali na mifuko ya kuhifadhia nafaka ambavyo vimezalishwa na vikundi vilivowezeshwa na TASAF.

Naibu waziri huyo  amesema mfumo unaotumiwa na TASAF katika kuwafikia walengwa wake unasaidia kwa kiwango kikubwa jitihada za serikali za kupambana na umaskini na pia kuwaongezea kipato wananchi hususani wanaoishi kwenye mazingira duni.

Aidha Mhe. Jaffu ametaka TASAF kujikita Zaidi katika kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye miradi ya uzalishaji mali huku wakizingatia  umuhimu wa kuweka akiba kwa njia ya vikundi ili hatimaye walengwa waweze kukuza mapato yao na kuondokana na umaskini.

Akiwa katika banda la TASAF Mhe. Jaffu na ujumbe wake wamepata maelezo ya namna TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini inavyotekeleza shughuli za kusaidia serikali katika kuondfoa kero ya umaskini hususani kwa  kaya za walengwa wa Mpango huo wanaokadiriwa kufikia Milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

Zifuatazo ni picha ya ziara ya Mhe. Jafu kwenye banda la TASAF kwenye maonyesho ya NANE NANE kwenye eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.

pic1

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jaffu akilakiwa na baadhi ya watumishi wa TASAF wakati alipotembelea banda la maonyesho ya Mfuko huo katika eneo la Nzuguni,nje kidogo ya mji wa Dodoma.

pic2

Naibu waziri wa TAMISEMI,Mhe. Jaffu ,akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Mawasiliano wa TASAF,Bi Zuhura Mdungi kwenye banda la maonyesho la TASAF.

pic3

Naibu Waziri wa TAMISEMI akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakikundi cha kutengeneza sabuni  na mafuta kwa kutumia zao la mwani kutoka Bagamoyo ambao wamewezeshwa na TASAF .

pic4

Baadhi ya watumishi wa TASAF walioko kwenye banda la maonyesho ya nane nane kwenye viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma wakitoa maelezo kwa naibu waziri wa TAMISEMI.

pic5

Mmoja wa wanakikundi cha uzalishaji asali kilichowezeshwa na TASAF kutoka Kongwa akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa TAMISEMI , Mhe. Suleiman Jaffu  na Naibu Waziri wa Kilimo  Mifugo NA UVUVI  wakati waliopotembelea banda la maonyesho  la TASAF kwenye viwanja vya Nzuguni,nje kidogo ya mji wa Dodoma.

pic6

Mmoja wa wageni waliotembelea banda ya TASAF kwenye maonyesho ya NANE NANE mkwenye manispaa ya Dodoma wakifurahia jambo baada ya kupata maelezo ya utekelezaji wa shughuli za TASAF.

pic7

Manaibu Waziri wa TAMISEMI na Kilimo ,Mifugo   na Uvuvi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waliotembelea banda la Ofisi ya Rais ambamo kuna banda la TASAF,TAKUKURU,MKURABITA na SEKRETARIETI YA  MAADILI YA VIONGOZI  kwenye viwanja vya nane nane ,Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.

 

 

 

Add comment


Security code
Refresh