Executive Director's Statement

It is with pleasure that I extend a warm welcome to all our readers to our newly redesigned TASAF website. This website offers information about TASAF, its work and.....

  • Studies
  • Publications

 

VULNERABLE GROUPS PLANNING FRAMEWORK DISCLOSURE - ENGLISH

Download  here   

 

VULNERABLE GROUPS PLANNING FRAMEWORK DISCLOSURE - SWAHILI

Download here 

Featured Interventions

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Ksiwani Unguja Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud amepongeza jitihada zinazofanywa na Mfuko huo katika kutekeleza maelekezo ya serikali ya kusaidia jitihada za kuwandolea kero ya umaskini wananchi.

Bwana Mahmoud ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema TASAF imekuwa kielelezo sahihi na cha kujivunia katika kutekeleza wa sera za kupambana na umaskini kwa kushajihisha wananchi kujiletea maendeleo kwa kutumia nguvu na raslimali zilizoko kwenye maeneo yao.

Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kianga unatekelezwa na Wananchi kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF kupitia utaratibu wa Mfuko huo wa kuendeleza miundombinu ya Afya,Elimu na Maji kwenye maeneo ya Walengwa.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema miradi iliyoibuliwa na Wananchi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF imeleta mageuzi makubwa katika maeneo mengi ya visiwa hivyo kufikia hatua ya baadhi yao kuzalisha bidhaa za kilimo kama vitunguu maji na hivyo kujiongezea kipato na kuukimbia umaskini uliokuwa unawakabili.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga amesema tangu Mfuko huo ulipoanzishwa na Serikali, umetoa mchango mkubwa katika kusaidia jitihada za kuboresha maisha ya wananchi huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo yametokana na sera sahihi za kupambana na umaskini zinazoratibiwa na serikali.

Bwana Mwamanga amesema TASAF imekuwa ikizingatia kwa kina maelezo ya Serikali yanayotilia mkazo pamoja na mambo mengine umuhimu wa wananchi wakiwemo Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuondokana na adha ya umaskini na kujiongezea kipato chao.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Serikali kupitia Mfuko huo imeamua kuboresha zaidi utekelezaji wa Mpango huo ili uweze kuwafikia wananchi wote wanaokabiliwa na Umaskini nchini huku msisitizo ukiwa ni kuibua shughuli za uzalishaji mali kwa kufanya kazi na kisha kulipwa kulingana na kazi watakayokuwa wameifanya.

Kwa Upande wao wananchi wa shehia ya Kianga wameishukuru Serikali kwa kuuwezesha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo kwenye shehia yao ukiwemo mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachowapunguzia adha ya kufuata huduma hiyo mbali na eneo lao.

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akihutubia wananchi wa Shehia ya Kianga,wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar (hawapo pichani) baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha Afya unaotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi wa eneo hilo.

pic2

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi ,Unguja Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud (aliyesisima nyuma ya meza) akiwahutubia wananchi wa Shehia ya Kainga baada ya kukagua ujenzi wa jengo la kituo cha Afya cha shehia hiyo unaojengwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi.

pic3

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Bw. Mahmoud akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.Mwamanga na maafisa wa serikali baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya-Kianga (nyuma yao)

pic4

Baadhi ya wananchi wa Shehia ya Kianga kisiwani Unguja wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga( hayupo pichani) baada ya kukagua jengo la kituo cha Afya kinachojengwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi.

pic5

Sehemu ya jengo la Kituo cha Afya Kianga katika mkoa wa Mjini Magharibi kinachoendelea kujengwa TASAF na Wananchi wa eneo hilo ambacho kitapunguza tatizo la kufuata huduma za Matibabu mbali na eneo lao.