WORLD BANK DIRECTOR FOR EXTERNAL COMMUNICATIONS AND PARTNERSHIP MS. HALEH BRIDI TOURED BAGAMOYO TASAF BENEFICIARIES

User Rating: 2 / 5

Star ActiveStar ActiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

The WORLD Bank (WB), Director for External Communications and partnerships, Ms. Haleh Bridi has reiterated their commitment on encouraging more development partners to support the Tanzania Social Action Fund (TASAF) programmes so as to enroll unreached poor households.

Ms.Bridi who was accompanied with TASAF Executive Director Mr. Ladislaus Mwamanga made the pledge during her official field visit to some of the TASAF Productive Social Safety Net Program (PSSN) at Kondo Village in Bagamoyo district, Coast region.

"We will continue to encourage other partners to join forces in funding the programme so that more poor people are covered," said Ms. Bridi.

Already groups such as the Department for International Development (DFID), the Organization of the Petroleum Exporting Countries (OPEC) and the Swedish International Development Cooperation Agency (SIDA) have agreed to extend funding in the programme.

Having witnessed implementation of the programme, the Director declared that their money was in good hands.

"We are very moved by the beneficiaries’ testimonies, as a woman and mother am very touched. I wish them all lots of courage and hope in moving forward," she said.

The TASAF Team Leader at the World Bank, Mr Muderis Abdulahi Mohammed, noted that similar programs are being implemented in countries such as Nigeria, Malawi and Ethiopia but among all Tanzania's quite unique.

"We commend the government of Tanzania for an outstanding performance. More emphasis should be put on monitoring," noted Mr. Mohammed.

He pointed out that by next year all cash transfers will be carried out electronically. On her part the Country Program Director at WB, Ms. Gayle Martin, said they are impressed with the scale and breathe of the programme.

"The money is being used productively as accordance to the requirements of program study. We are glad that we have witnessed individual change that acts a result to the development of the country," she said.

Earlier, the Village Chairperson of Kondo Village pointed out that PSSN programme has enabled his people to come out from poverty through cash transfers, public works such as rehabilitation of community feeder roads and mangrove tree planting.

Among others include participation of the beneficiaries in establishing savings and investment groups.

Mr. Kondo cited challenges such as availability of poor households that have not been reached, lack of health facilities and inadequate teachers' houses in the village.

Below are the photographs taken during the visit

pic1

pic2

pic3

pic4

pic5

pic6

pic7

pic8

pic9

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATEMBELEA OFISI ZA TASAF JIJINI DAR ES SALAAM

User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Wajumbe wa kamati ya Baraza la wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu ya baraza la wawakilishi – Zanzibar wameanza ziara ya siku mbili ya kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- kwa lengo la kujifunza utendaji kazi wa mfuko huo ambao pia hutekeleza miradi yake huko Unguja na Pemba.

Wakiwa katika ofisi za Makao makuu ya TASAF wajumbe hao wamepewa taarifa ya miradi iliyotekelezwa na taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.Katika taarifa hiyo jumla ya miradi ya maendeleo 12,347 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 430 imetekelezwa kote nchini kwa kuwashirikisha wananchi .

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa kamati hiyo,Mhe. Omar Seif Abed amesema kazi zilizofanywa na TASAF zimeibua hamasa kwa wananchi kujiletea maendeleo na kupongeza utaratibu wa Mfuko huo kuwashirikisha wananchi katika uibuaji na utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yao.

Aidha Mwenyekiti huyo ametoa changamoto kwa TASAF kuona namna inavyoweza kufuatilia miradi iliyoitekeleza hata baada ya kuwakabidhi wananchi au halmashauri ya wilaya ili iwe endelevu.

Wajumbe hao watapata fursa ya kutembelea miradi ya TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani ambako watakutana na baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za Wajumbe wa Kamati hiyo walipokuwa katika kikao Makao Makuu ya TASAF

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Mr.Ladislaus Mwamanga akiwakaribisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar TASAF Makao Makuu

pic2

Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wakipitia taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya TASAF 

pic3

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Kisiwani Zanzibar Mhe. Mihayo Juma Nhunga aliyesimama akitoa nasaha katika ziara ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotembelea Makao Makuu ya TASAF jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo.

pic4

Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo wa TASAF, Mr. Amadeus Kamagenge aliyesismama akitoa  taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Mfuko huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 

 

 

 

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TASAF KISIWANI PEMBA

User Rating: 4 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Inactive

Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala Bora na Serikali za Mitaa imetembelea miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Unguja na Pemba na kuridhishwa na hatua ya Maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wake kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba akizungumza na wananchi wa shehia ya Ndagoni Kisiwani Pemba baada ya kukagua ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi ya baharini yasiathiri mashamba ya wananchi, ametaka walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutumia fursa ya Mpango huo kupunguza kero ya umaskini.

Ametoa Mfano wa Miradi iliyojengwa kwa ufanisi kuwa ni pamoja na matuta ya kuzuia maji chumvi ,upandaji wa mikoko, uchimbaji wa mitaro ya maji ,uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba, na ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati miradi iliyotekelezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa utaratibu wa ajira ya muda kisiwani Unguja na Pemba.

Kwa kutengeneza matuta ya kuzuia maji ya chumvi, walengwa hao wa TASAF wameweza kuokoa zaidi ya hekta 200 za mashamba ya mpunga katika shehia ya Ndagoni kisiwani Pemba kwa njia ya ushiriki kwenye ajira ya muda .

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema serikali inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa shughuli za TASAF ili kuziboresha zaidi kwa manufaa ya wananchi.

Aidha Waziri huyo ameiagiza TASAF kuviimarisha zaidi vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza vipatavyo 876 kwenye shehia 78 vilivyoundwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kisiwani humo kwa kuvipatia nyenzo muhimu hususani elimu na vitendea kazi ili vikundi hivyo viwe endelevu.

pic1

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mheshimiwa Mwita Mwikabe Waitara mbunge wa Ukonga amesema mfumo wa kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya kuibua na kutekeleza miradi unaotumiwa na TASAF umeamusha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za Maendeleo na kutatua kero zinazowakabili badala ya kuitegemea serikali pekee.

Wakitoa ushahuda wa namna wanavyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika shehia ya Ndagoni na Shidi kisiwani Pemba ,baadhi ya walengwa wa Mpango huo wamewaambia wajumbe wa kamati hiyo ya bunge kuwa uwezo wao wa kuhudumia watoto hususani wanafunzi umeongezeka na hivyo kuboresha mahudhurio yao shuleni na hata kwenye vituo vya afya ili kutimiza masharti ya Mpango.

Hata hivyo baadhi ya walengwa hao wamesema kwa sasa wanakabiliwa na soko la bidhaa wanazozalisha hususani mboga mboga kutokana na ongezeko la bidhaa hiyo kwenye maeneo yao.Mpango wa Kunusuru Kaya masikini unaotekelezwa na TASAF nchini kote pia umeweka mkazo katika shughuli za usalishaji mali kwa walengwa ili waweze kukuza kipato .

Zifuatazo ni picha za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala Bora na Serikali za Mitaa wakati wa ziara yao kisiwani Pemba kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.

pic2

pic3

pic4

pic5

pic6

pic7