NORDIC Partners' Mission to Tanzania

User Rating: 4 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Inactive

THE Nordic partners’ mission to Tanzania is pleased with the Tanzania Productive Social Safety Nets (PSSN) under the Tanzania Social Action Fund-TASAF- aimed at reducing abject poverty among poor households.

PSSN which is carried out by the government under the Tanzania Action Social Fund (TASAF), they said is the right way to improve food security at household level and help alleviate poverty the move which is implemented in other countries.

pic1

 

The delegation with representatives from Sweden, Norway, Denmark, Finland and Iceland has been in the country for a week-long mission to Tanzania, holding several meetings with different stakeholders.

Tanzania’s UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez speaking on behalf of the delegation described the TASAF initiatives as well designed and intensive programmes which not only benefit the target people, but also the entire community.

"This is commendable in Tanzania and other countries in the world and the government should be proud of the well-designed projects," said the UN Leader after visiting the projects implemented by TASAF at Msalato Ward, few kilometers off Dodoma Town yesterday.

pic2

 

He observed that the Nordic countries have been key partners to the UN in development and humanitarian activities.

He added that their visit to Tanzania comes at the right time when the UN and the government have developed their five-year plan for eradicating poverty, addressing climate change and ensuring sustainable development.

The delegates are in the country to strengthen their collaboration with the UN in support of the Global Goals and strategic development priorities of the Tanzanian government.
According to Mr Rodriguez, the UN team in Tanzania is supporting the government to scale-up PSSN programme and strengthen coordination of social protection intervention across sectors.

Ms. Kit Clausen, Senior Adviser, Danish representation to the UN in New York, who was part of the team said, “It is really impressive to see what the government is doing to change the livelihoods of poor people”.

Ms. Melina Benjamin, who is one of the TASAF programme beneficiaries, says the programme has helped her to pay school fees for her grandchildren, adding that she now get three meals per day unlike in the past before the programme when she used to have just a meal per day.

"TASAF has helped me to join National Health Insurance Fund which enables me to get medical treatment," she said, noting that her life has completely changed.

For Agnes Kundeli, another TASAF beneficiary at the village, said TASAF has helped her to start poultry farming thus to get income after selling chicken, saying the TASAF programme has tremendously improved her life.

Dodoma municipal council is among seven councils of Dodoma Region implementing PSSN program aimed at enabling poor household increase incomes and opportunities while improving consumption.

pic3

 

The district’s Project Area Authorities (PAA) launched in 2014 cover 73 villages with 7802 poor households. At least 12,272 beneficiary households were targeted and 8,100 beneficiary’s households were enrolled and currently 7,664 are receiving cash transfer.
Establishment of a Productive Social Safety Net (PSSN) in TASAF III has helped TASAF beneficiaries to participate in public works aimed at putting up infrastructures in the area of education, health and water to improve social services.

The Government started to implement the PSSN with a view to putting in place the building blocks of a permanent national social safety net system in the country.

pic4

 

PSSN provides support to strengthen the institutional capacity at various levels to implement and monitor safety net programmes.

The development objective of the first phase of PSSN is to create an efficient, well-targeted productive social safety net system for the poor and vulnerable section of the population, with building incentives for them to use health and education services and opportunities to earn additional income on public works projects.

The Government in 2013 made the decision to scale up the PSSN to support 1.2 million households. PSSN scale up is geared towards contributing to the achievement of Millennium Development Goals (MDGs), particularly MGD 1 on reduction of extreme poverty and hunger by half by December 2015.

TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active

Wadau wa Maendeleo wanaoshirikiana na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN- wameanza mkutano jijini Dar es salaam kupitia mafanikio ya utekelezaji wa Mpango huo.

Akifungua Mkutano huo wa siku moja, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo amesema Serikali inathamini na kutambua mchango wa wadau hao wa maendeleo katika kusaidia jitihada za kutokomeza umaskini miongoni mwa wananchi.

Bwana Ilomo amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF umekuwa wa mafanikio ya kuridhisha ambapo Zaidi ya kaya maskini Milioni Moja zimetambuliwa na kuorodheshwa kwenye Mpango huo nchini kote.

Aidha Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais amebainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa Mpango huo serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake ili malengo yake yaweze kupatikana kwa haraka na kuwanufaisha walengwa na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Bwana Ilomo amezungumzia hatua zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya watu waliopenyezwa kwenye Mpango bila kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuziondoa takribani kaya 30,000 zilizokuwa zimeandikishwa kinyume cha kanuni za Mpango.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko huo umefanikiwa kulipa walengwa wa Mpango kwa awamu 17 nchini kote ambako katika maeneo mengi ya Mpango tayari mafanikio yameanza kuonekana ikiwemo walengwa kuboresha maisha,kusomesha watoto na hata kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa lengo la kujiongezea kipato.

Wadau hao wa Maendeleo kesho watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini na kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kuona namna wanavyonufaika na ruzuku itolewayo na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

 

Zifuatazo ni picha za tukio la ufunguzi wa mkutano wa TASAF na wadau wa Maendeleo uliofunguliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo jijini Dar es salaam.

mission1

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akizungumza na wadau wa Maendeleo Ikulu jijini Dar es Salaam

mission2

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akifungua mkutano wa wadau wa maendeleo ulioandaliwa na TASAF

mission3

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akitoa maelezo kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo jijiji Dar es salaam

mission4

Baadhi ya wadau wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa wadau awa maendeleo jijini Dar es salaam iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo (hayupo pichani)

mission7

Wadau wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo baada ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

 

 

 

 

 

 

TASAF YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa Menejimenti ya taasisi hiyo kukutana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii unaotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini , unatoa huduma kwa Zaidi ya Kaya Milioni Moja na Lakini Moja nchini kote jukumu iliyopewa na serikali katika jitihada zake za kupambana na Umaskini nchini..

Imearifiwa katika kikao hicho kuwa mafanikio makubwa yameanza kujitokeza kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo wengi wao wameanza kujiwekea misingi ya kupunguza umaskini kwa kuwa na uwezo wa kusomesha watoto,kupata huduma za afya,kuwa na uhakika wa lishe na kuongeza uchumi wao.

Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini pia umeanza kusisimua hamasa ya walengwa wa Mpango huo kuboresha maisha yao kwa kiwango cha kuanza kuboresha makazi yao kwa kujinunulia mabati na kuezeka nyumba,kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku wa kienyeji,mbuzi na hata nguruwe.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga amesisitiza watumishi wa Mfuko huo kuendeleza jitihada za kuwahudumia wananchi na hususani walengwa wa Mpango kwa kuzingatia taratibu na kanuni za utumishi wa umma kama zinavyoelekeza.

Zifuatazo ni picha za watumishi wa TASAF wakiwa kwenye ukumbi wa mikutanowa taasisi hiyo maarufu kama “Mlimani City conference hall” ulioko makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es salaam.

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ( aliyeshika kipaza sauti) akitoa ufafanuzi juu ya moja ya masuala yaliyoulizwa na wafanyakazi (hawapo pichani) katika kikao cha kufunga wiki ya utumishi wa umma yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar esa salaam.

pic2

Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika Mkutano wa kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma uliojadili namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

pic3

Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakiwa katika kilele cha wiki ya Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Mikutano wa Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam.

pic4

Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Bwana Ladislaus Mwamanga( hayupo pichani) kujadili uboreshaji wa huduma za mfuko huo katika utoaji wa huduma kwa wananchi.