WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA APONGEZA MCHANGO WA TASAF KATIKA KUPAMBANA NA UMASIKINI NCHINI.

User Rating: 2 / 5

Star ActiveStar ActiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Huruma Mkuchika amesema serikali itaendelea kuunga mkono mchango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kutatua kero zinazowakabili wananchi katika kupambana na umasikini ili vita hiyo iwe endelevu .

Mheshimiwa Mkuchika amesema jambo muhimu kwa TASAF ni kuhakikisha kuwa walengwa wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wanafikiwa na kunufaika na huduma za mfuko huo huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili mema katika utendaji kazi wa wadau wote wanaohusika na utekelezaji wa Mpango huo .

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF zilizowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga mjini Dodoma, Waziri Mkuchika ameuagiza uongozi wa TASAF kuhakikisha kuwa unawatumia kikamilifu Maafisa maendeleo ya Jamii walioko katika maeneo mbalimbali nchini kuhamasisha shughuli za maendeleo na kupambana na umasikini.

“tunao maafisa maaendeleo ya Jamii nchini kote,lakini nina wasiwasi na namna wanavyotumiwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,naagiza TASAF mtumie vizuri hazina hiyo ya wataalamu katika utendaji kazi wenu” ameagiza Waziri Mkuchika.

Aidha Waziri huyo ameitaka menejimenti ya TASAF kuhakikisha kuwa inaandaa mipango thabiti katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kipindi kirefu huku akisisitiza kuwa walengwa wa Mpango huo wanapaswa kuwekewa mazingira yatakayowawezesha kujitegemea hata baada ya kuondolewa kwenye shughuli za Mpango.

Akitoa taarifa ya utekelezaji,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mfuko huo umeendelea kuwajengea msingi wa kujitegemea walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini  nchini kote,kazi ambayo amesema imefanyika kwa mafanikio makubwa.

Walengwa wengi hivi sasa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwenye maeneo yao huku akitaja mafanikio makubwa katika utekelezaji wa masharti ya elimu na afya kwa walengwa jambo ambalo amesema linaendelea kusaidia juhudi za serikali za kupambana na adua ujinga na maradhi.

“Kumekuwa na mwitikio mkubwa katika kuwapeleka watoto kutoka kaya masikini kupata elimu na huduma za afya, kwani hayo ni miongoni mwa  masharti ya Mpango, na hyo kwetu ni mafanikio makubwa” amesisitiza Bwana Mwamanga.Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mfuko huo kwa sasa unakabiliwa na changamoto ya kufikia takribani asilimia 30 ya vijiji ambavyo havikufikiwa katika awamu inayokaribia kukamilika, hivyo jitihada zaidi zinafanywa ili kupata fedha za kukamilisha vijiji hivyo katika awamu itakayofuata.

Zifiatazo ni picha za tukio hilo.

pic1

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Mhe. George Mkuchika (aliyevaa tai nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislau Mwamanga,ofisi kwa Waziri mjini Dodoma.

pic2

Mheshimiwa Mckuchika akitazama nakala za vipeperushi,taarifa na majarida yenye taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF,Ofisi kwake mjini Dodoma.

pic3

pic4

Waziri Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na Utumishi wa Umma ,baada ya kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF ofisini kwake mjini Dodoma, aliyevaa Kaunda suti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga.

 

 

WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA NA MAAFISA WA SERIKALI NA TASAF MJINI DSM.

User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa Serikali na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wanakutana jijini Dar es salaam baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.

Vikao kazi hivyo vilivyoanza kwenye makao makuu ya TASAF mjini Dar es salaam vitapitia taarifa zilizopatikana kwenye maeneo yaliyotembelewa na wadau hao wa maendeleo na maafisa wa serikali ili kuona Mafanikio na Changamoto za utekelezaji wa  Mpango wa kunusuru kaya Masikini unaohudumia takribani kaya milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

Wakiwa katika maeneo hayo ya utekelezaji wajumbe walipata fursa ya kukutana na baadhi ya walengwa wa Mpango huo na kuona shuhuda mbalimbali za namna Mpango huo unavyoendelea kupunguza adha ya umasikini kwa kutumia fedha wanazozipata kuanzisha shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato.

Miongoni mwa miradi iliyoanzishwa na walengwa ni pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi,nguruwe na hata  ng’ombe wa maziwa  na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za matofali na kuezeka kwa mabati tofauti na hali waliyokuwa wakikabiliwa kabla ya kuingizwa kwenye shughuli za Mpango.

Vikao kazi hivyo vinavyoambatana na ziara kwenye maeneo ya Utekelezaji wa Mpango hufanywa kila baada ya miezi SITA kwa lengo la kuboresha huduma kwa walengwa na kusaidia nia ya serikali ya kujenga mazingira  wezeshi kwa wananchi kukuza mapato yao kwa kuanzisha miradi midogo midogo kulingana na mazingira yao.

Mikoa ambayo wadau hao wa maendeleo na maafisa wa serikali na TASAF wametemebelea ni pamoja na Tabora, Kigoma, Njombe,Ruvuma,Kilimanjaro, Morogoro, na Zanzibar.Baada ya vikao hivyo taarifa ya maendeleo ya utekelezaji na mapendekezo yakayofikiwa itawasilishwa serikalini.

Zifuatazo ni picha za wajumbe wa vikao hivyo vinavyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano makao makuu ya TASAF jijini Dar es salaam.

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga (kulia) akiwa na Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika benki ya Dunia Bw. Muderis Mohamed wakiwa katika kikao kazi hicho.

pic2

Mmoja wa maafisa wa TASAF Bw. Hamis Kikwape (aliyeshika kipaza sauti) akiwasilisha taarifa baada ya kurejea kutoka Zanzibar na Morogoro akiwa na wadau wa maendeleo.

pic3

Baadhi ya wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha pamoja cha kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

pic4

Mmoja wa maafisa wa TASAF Bi. Tumpe Lukonge (aliyeshika kipaza sauti) akiwasilisha taarifa ya ziara kwa wajumbe wa kikao kazi cha wadau wa maewndeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF ,kinachojadili utekelezaji wa  Mpango wa Kunusuru Kaya masikini.

 pic5

Baadhi ya wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha pamoja cha kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

 

WADAU WA MAENDELEO NA MAAFISA WA SERIKALI KUTEMBELEA WALENGWA WA TASAF.

User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Baadhi ya watendaji wa Serikali na Wadau wa Maendeleo wanaanza ziara katika maeneo mbalimbali ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- kukutana na walengwa wa Mpango huo na kuona mafanikio na changamoto za utekelezaji wake.

Akitoa maelezo kabla ya kuanza kwa ziara hizo zitakazofanyika katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Kigoma, Tabora, Singida, Kilimanjaro ,Morogoro na Zanzibar ,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru serikali na wadau wa maendeleo kwa mchango mkubwa wa kufanikisha shughuli za Mpango huo unaohudumia zaidi ya kaya masikini MILIONI MOJA na Laki MOJA nchini kote.

Hata hivyo Bwana Mwamanga amesema licha ya kuweko kwa mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Mpango, bado kuna asilimia 30 ya vijiji nchini ambavyo havijafikiwa na huduma za Mpango jambo linaloendelea kulalamikiwa na wananchi ambao hawajafikiwa na Mpango huo na hivyo amesema serikali kupitia TASAF inalifanyia kazi kwa karibu suala hilo.
Aidha katika maelezo ya utekelezaji wa Mpango huo yaliyowasilishwa na Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi imeonyeshwa kumekuwa na mafanikio katika kubadili fikra na za kaya za walengwa katika kupambana na umasikini kwa kutumia huduma za Mpango huo mkubwa kupata kutekelezwa nchini .

Shughuli za ziara na majadiliano kati ya serikali,wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF hufanyika kila baada ya miezi sita kuona namna utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unavyoendelea kwa kukutana na walengwa ,viongozi,wataalam na kuwasikiliza namna huduma za Mpango huo zinavyosaidia jitihada za serikali za kupunguza adha ya umaskini kwa wananchi

Zifuatazo ni picha za ufunguzi wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya TASAF mjini Dar es salaam.

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF- Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akifungua kikao kazi kati ya maafisa wa serikali na wadau wa maendeleo (hawapo pichani ) kwenye ukumbi wa TASAF mjini Dar es salaam.

pic2

Moja wa maafisa wa Benki ya Dunia,ambaye pia huratibu shughuli za TASAF (TTL) katika benki hiyo , bw. Muderis Mohamed (aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na serikali mjini Dar es salaam.

pic3

Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa TASAF ,Bi. Zuhura Mdungi (aliyesimama) akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- PSSN- kwenye mkutano wa wadau na serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF ,mjini Dar es salaam.pic4

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa maendeleo, serikali na watumishi wa TASAF –wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo kupata maelezo ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini kabla ya kuanza ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali nchini kukutana na walengwa na viongozi .

pic5

pic6

Baadhi ya watumishi wa TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia maelezo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini,kabla ya ziara ya maeneo kadhaa nchini kuona utekelezaji wa Mpango huo.

pic7