TASAF SHINES AGAIN

User Rating: 4 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Inactive

TANZANIA Social Action Fund –TASAF- came first among 19 basket funds following an analysis by the National Economic Empowerment Council (NEEC) to establish contribution to members of the public to alleviate poverty. TASAF scored 81 points to become a winner in its category.

TASAF has been carrying out a number of programmes including Productive Social Safety Net (PSSN) and Community Based Conditional Cash Transfer (CBCCT).The programmes aim to help people living in abject poverty to engage in income generating activities. Currently, PSSN saves more than 1.1 MILLION poor households from both Tanzania mainland and Zanzibar.

pic1

TASAF Executive Director, Mr. Ladislaus Mwamanga receive a trophy from Minister Jenister Mhagama after TASAF emerging a winner among 19 basket funds to empower Wananchi in poverty alleviation in Tanzania. 

The award was given during 2nd Economic Empowerment Forum in Tanzanian Capital City –Dodoma.

Speaking after presenting an award to staff members, TASAF executive Director Mr. Ladislaus Mwamanga pointed out that, the victory should motivate them to work even harder for the benefit of the nation and especially poor households who are in the PSSN program.

pic2

TASAF Executive Director displays a trophy and Certificate after his organization emerged a winner among basket funds in poverty alleviation in the country.

“It’s yet another testimony of how TASAF is seriously working to meet the government’s policy against poverty” he emphasized Mr. Mwamanga.

pic4

TASAF workers in a group photograph after receiving a trophy at their headquarters in Dar es Salaam.

According to NEEC a number of criteria were used to analysis projects including the value to the public, a number of beneficiaries based on gender, sectors impacted by the projects and other services provided by the funds. The analysis also focused on the funds which offer grants and those offer loans or facilitate people to access loans,” observed the statement.

Other basket funds were the National Entrepreneurs Development Fund (NEDF), Mwananchi Empowerment Fund (MEF), Small and Medium Enterprises Credit Guarantee Scheme (SME-CGS), Contractors Assistance Fund (CAF) and Tanzania Education Fund (TEF).

Others are Agricultural Inputs Trust Fund (AGITF), Presidential Trust Fund (PTF), Youth Development Fund (YDF), Women Development Fund (WDF), SELF Microfinance, UTT Microfinance, Private Agricultural Sector Support (PASS  Trust Fund) and JK Fund.The Kilimo Kwanza Catalytic Fund (KKCF), Rural Energy Agency (REA) and Tanzania Forest Fund (TaFF).

 

TASAF YAIBUKA KIDEDEA KATIKA SHUGHULI ZA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI.

User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- umeibuka mshindi wa kwanza kati ya Mifuko 19 inayojihusisha na shughuli za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa mwaka 2017 nchini.

Ushindi huo umetangazwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi –NEEC- baada ya tathimini ya kutambua mchango wa Mifuko hiyo iliyoanzishwa na serikali kwa lengo la kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa wananchi hususani wale wa kipato cha chini ili waweze kuboresha maisha yao.

Taarifa iliyotolewa na NEEC imeonyesha kuwa TASAF imepata alama 81 ikifuatiwa na Mfuko wa SELF Microfinance uliopata alama 71 huku Mfuko wa Kuwaendeleza Wajasiliamali Wananchi NEDF ukipata alama 70 na kushika alama ya tatu.

Miongoni mwa vigezo vilivyoupa ushindi Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ni pamoja na Idadi kubwa ya wanufaika wa huduma zake kutoka Kaya zipatazo MILIONI MOJA NA LAKI MOJA ,uwezo wake wa kuwafikia walengwa nchini kote,thamani ya fedha zilizowanufaisha walengwa  na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli zake kwa wakati.

Akizungumza na Wafanyakazi kufuatia ushindi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amewahimiza waendelee kujituma zaidi katika utendaji kazi,ili mchango wao katika vita dhidi ya umasikini uwe endelevu na wenye kutoa tija kwa taifa.

Bwana Mwamanga amesema ni vema wakati wote wa utekelezaji wa shughuli , watumishi wa TASAF waendelee kuzingatia maadili bora ya utumishi wa umma, na kuwapa huduma stahiki wananchi na kutekelezaji maagizo ya serikali ya uboreshaji wa huduma kwa wananchi ili kuwapunguzia kero ya umasikini.

Zifuatazo ni picha za tukio hilo.

pic1

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge ,Kazi, Vijana na Walemavu Mhe. Jennista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga Cheti cha Ushindi wa Kwanza katika ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini.

pic2

pic3

pic4

Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakifurahia ushindi wa kwanza ambao Mfuko huo umepata kwa mwaka 2017 kati ya mifuko 19 inayoshughulikia uwezeshaji wananchi kiuchumi.

 

TASAF NA WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA MJINI DSM.

User Rating: 2 / 5

Star ActiveStar ActiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- na wadau wa maendeleo wameanza mkutano wa kutathimini utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kipindi cha miezi SITA iliyopita.

Mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi  wa mikutano wa  ofisi za TASAF mjini Dar es salaam pia unawajumuisha maafisa wa serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar,pamoja na mambo mengine umefahamishwa juu ya mafanikio na changamoto zilizopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini kwa kipindi cha kuishia mwezi Marchi mwaka huu.

Katika mawasilisho  ya shughuli zilizotekelezwa na TASAF katika kipindi kilichopita, imeonyeshwa kuwa zaidi ya kaya milioni moja  za walengwa zimeendelea kunufaika na Mpango kupitia ruzuku na utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoibuliwa na walengwa kupitia utaratibu wa ajira ya muda ambapo hulipwa ujira baada ya kutekeleza kazi hizo.

Aidha taarifa hiyo imeonyesha kuwa  kumekuwa na mwitikio chanya wa walengwa katika kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kutumia fedha zinazotolewa na TASAF chini ya utaratibu wa uhawilishaji fedha, na hivyo kusaidia kwa kiwango kikubwa ongezeko la kipato kwa kaya zilizoandikishwa kwenye Mpango.

Mafanikio mengine yaliyoonyeshwa ni ongezeko la mahudhurio ya  watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kutoka katika kaya za walengwa kupata huduma za kliniki kwa lengo la kuboresha afya na makuzi yao pamoja na kuongezeka  kwa mahudhurio shuleni kwa watoto wanaotoka kwenye kaya za walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini.

Katika kuboresha zaidi huduma kwa walengwa, TASAF kwa kushirikiana na idara nyingine za serikali imeandaa utaratibu wa kuanza kutoa ruzuku ya fedha kwa njia ya kielektroniki  ambapo majaribio yataanza katika baadhi ya maeneo ya Utekelezaji wa Mpango huo.

Wadau hao wa Maendeleo baada ya kuhudhuria mkutano huo wa siku moja watapata fursa ya kutembelea maeneo ya utekelezaji  wa Mpango huko Zanzibar,Itirima,Magu,Lindi  Longido ambako watawatembelea walengwa wa Mpango kuona namna wanaoendelea kunufaika na fedha zinazotolewa katika jitihada za serikali kupitia TASAF katika kuwaondolea wananchi kero ya umaskini.

Zifuatazo ni picha za washiriki wa mkutano huo wa wadau wa maendeleo ,baadhi ya maafisa wa serikali na watumishi wa TASAF unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii jijini Dar es Salaam

 

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akifungua mkutano wa wadau wa maendeleo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo jijini Dar es salaam.

pic2

Msimamizi wa shughuli za TASAF (Benki ya Dunia) Bwana Muderis  Mohamed  (aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na TASAF .

pic3

Baadhi ya wadau wa Maendeleo na Maafisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF – wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini.

pic4

pic5

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wadau wa maendeleo na TASAF (picha ya juu na chini ) wakiwa kwenye mkutano ulioanza leo kujadili utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini.

pic6