Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Benki ya Dunia yafurahishwa na matumizi ya Ruzuku ya Uzalishaji Mtwara


Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia, Stanley Magesa na Faith Msechu wakizungumza na wanufaika wa Ruzuku ya Uzalishaji inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kaya za walengwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Wanufaika hao wamepata ruzuku baada ya kila mmoja kuandaa mpango rahisi wa biashara na kujihusisha katika shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato huku wakishauriwa na kukufuatiliwa na watumishi wa ughani wa Halmashauri.

Wakizungumza baada ya kutembelewa, wanufaika wa Ruzuku ya Uzalishaji walisema wameimarika kiuchumi na sasa wako tayari kujitegemea.