Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Kuinua Kaya (Huduma na Manufaa)

Madhumuni ya Kipindi cha Pili ni kuongeza fursa za kujiongezea kipato na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kaya za walengwa na kulinda maslahi ya watoto wao.

Kipindi cha Pili kitafikia malengo yake kwa kutekeleza shughuli mbalimbali kupitia sehemu kuu tatu ambazo ni uhawilishaji fedha ambao utaongeza kipato cha kaya na kuwekeza katika afya na elimu ya watoto, kuinua uchumi wa kaya kwa kujenga uwezo kwa kaya katika utunzaji rasilimali na kutengeneza njia mbadala na endelevu za ajira na kushiriki katika kazi za jamii na kupata kipato cha ziada kwa matumizi ya kaya kama chakula na kugharamia mahitaji mengine ya msingi na wakati huo huo wakiboresha miundombinu katika jamii na kupata ujuzi na stadi za maisha

UHAWILISHAJI FEDHA WENYE MASHARTI

Uhawilishaji fedha umegawanyika katika makundi matatu:

  • Kwanza ni uhawilishaji wenye masharti ya kushiriki katika vikundi vya kuweka akiba kwa kaya zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi. Kaya zenye watu wasio na uwezo wa kufanya kazi zitapata uhawilishaji usio na masharti. Kwa wale wenye uwezo wa kufanya kazi wataendelea kuhawilishiwa fedha bila masharti wakisubiri kuandikishwa kwenye mpango wa ajira za muda. Mara tu wanapoanza kutekeleza miradi ya ajira za muda, hawataendelea kupokea uhawilishaji wa msingi.
  • Pili ni uhawilishaji fedha kwa makundi maalum: Huu hutolewa kwa kaya zenye watoto hadi umri wa miaka 18 na kaya zenye mtu/watu wenye ulemavu.
  • Tatu ni uhawilishaji wa masharti: Uhawilishaji huu hutolewa kwa kaya zenye watoto kwa kutimiza masharti ya afya au elimu. Masharti ya afya ni kwa watoto chini ya miaka mitano kuhudhuria kliniki na wenye umri wa kwenda shule kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita kuhudhuria masomo.